Aliyekuwa Mbunge wa Same Mashariki na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anne Kilango Malecela wa Serikali ya Awamu iliyopita ambaye jana aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ameeleza sababu zilizopelekea Rais John Magufuli kuliona jina lake katika nafasi hiyo.

Akiongea na kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm, amesema kuwa historia yake ya utendaji kazi kwa miaka 15 aliyokuwa Bungeni na Rais Magufuli ndio chanzo cha kumuamini kuwa anaweza kushika nafasi hiyo.

“Mungu ni mwema, sikuwa na hili wala lile, nimekaa Bungeni miaka 15 na Mh Rais akiwa kama Mbunge, kwahiyo alikuwa anaona utendaji wangu, kupambana na kero za wananchi na jinsi nilivyo na jitihada,” alisema.

Hata hivyo, Mama Malecela ambaye alikuwa mpambanaji mkubwa kwenye bunge la Kumi akiwa kama Mbunge na baadae Naibu Waziri kwa kipindi kifupi kilichosalia cha awamu ya nne, alieleza kuchezewa ndivyo sivyo kwenye uchaguzi uliopita uliomuondoa jimboni.

“Unajua wanaosema tunabebwa tulianguka kwenye uchaguzi, watazame kwa ustandi wengine tuliangushwa, naahidi kuzikabili na kauli mbiu ya kazi tu kuitumikia Shinyanga” Mama Malecela anakaririwa.

Muro Amjibu Haji Manara Kwa Kumtaka Ajivunie Historia Yake
Zitto Kabwe apandishwa kizimbani kujibu Sakata la Escrow