Makamu wa Rais wa FC Barcelona, Rafa Yuste, amesema hana uhakika wa asilimia 100 kama Mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Ansu Fati atasalia klabuni hapo, licha ya kufahamu kuwa bado Mkuu wa Benchi lao la Ufundi Xavi Hernandez anamuamini.

Taarifa kutoka mjini Barcelona nchini Hispania zimekuwa nyingi kuhusiana na hatma ya Fati ndani ya FC Barcelona kutokana na kutokuwa na nafasi wa kudumu katika kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Camp Nou.

Hivi karibuni, baba mzazi wa Mshambuliaji huyo alizungumzia juu ya ishu ya mtoto wake kusugua benchi na kutopewa nafasi ndani ya kikosi hicho.

Xavi ameweka wazi kuwa: “Ninamuamini Ansu Fati na Ferran Torres wamekuwa wakijituma na kupambania nafasi zao ndani ya timu.”

Makamu wa Rais wa Barcelona, amesema: “Siwezi kuwa na uhakika wa asilimia 100 kuwa Ansu Fati atakuwepo kwa sababu haitegemeani na mimi, lakini naweza kusema Xavi bado anamuamini.”

“Nilishamwambia Ansu anatakiwa kufanya maamuzi juu ya hatma yake. Lakini sipendi kuona kipaji kutoa La Masia kinaondoka ndani ya Barcelona.”

Meneja AC Milan amwagia sifa Rafael Leao
Benjamin Pavard ngoma nzito Ujerumani