Pambano la uzito wa juu baina ya Anthony Joshua na Carlos Takam lililopigwa usiku wa kuamkia leo mjini Cardiff limemalizika kwa Joshua kutetea ubingwa wake wa WBA ‘super’ na IBF baada ya kumpiga Carlos Takam kwa TKO ‘Technical knock out’ raundi ya 10.

Joshua mwenye umri wa miaka 28 aliumia pua raundi ya pili baada yakugongana kichwani na mpinzani wake lakini hatua kwa hatua alizidi kuimarika na kufanikiwa kumchapa Carlos Takam raundi ya 10.

Huu ni ushindi wa 20 mfurulizo kwa Anthony Joshua kushinda kwa ‘knock out’ baada ya kumtwanga Wladmir Klitschko mnamo mwezi Aprili katika uwanja wa Wembley.

Raundi ya 10 Joshua alionekana kumshambulia Takam kwa nguvu huku makonde mengi yakimpata Takam moja kwa moja na mwamuzi wa pambano hilo kuamua kumaliza pambano jambo ambalo liliwashangaza wengi wakidai mwamuzi alimaliza pambano mapema baada ya kuona Takam akizidiwa.

Anthony Joshua retains world titles after stopping Carlos Takam in 10th round

 

 

Video: Lissu sasa kimya kimya, siri nzito maiti zinazookotwa baharini
Mwanri azicharukia halmashauri Tabora