Bingwa wa dunia wa masumbwi ya uzito wa juu, Anthony Joshua amemvaa bondia Tyson Fury akitamba kumuaibisha ulingoni.

Joshua ambaye hana historia ya kushindwa pambano lake, akishinda mapambano yote 20 kabla ya raundi ya mwisho (Knock Outs), amesema kazi ya kumpiga Tyson ni kazi rahisi kwakuwa ni ‘mwehu’.

“Kama mtu akiwa mwehu au mpumbavu kwenye biashara, anakuwa hivyo pia hata anapopanda ulingoni,” alisema Joshua.

“Kazi ya kumpiga ni rahisi, ni kazi kama zilivyo kazi nyingine rahisi, haitakuwa tofauti na ilivyokuwa kwa Wladimir Klitschko ,” aliongeza.

 

Joshua ambaye anatafutwa na mabondia wengi wa uzito wa juu ili kufanya biashara kubwa kwa kuwa kivutio cha maelfu ya watu, amekuwa akitoleana maneno na Tyson kiasi cha kuaminika kuwa huenda mwaka 2018 wawili hao wakakata mzizi wa fitina.

Tyson ambaye alikuwa amestaafu masumbwi, alimualika Joshua ulingoni baada ya kuona alivyomzima Klitschko.

LIVE: Rais Magufuli akihutubia katika uzinduzi wa hospitali ya taaluma na tiba, Mloganzila
LIVE: Rais Magufuli akizindua hospitali ya taaluma na tiba, Mloganzila