Bondia wa Uingereza Anthony Oluwafemi Olaseni Joshua anatarajiwa kutetea mataji yake ya IBF na WBA atakapovaana na Carlos Takam baada ya Kubrat Pulev raia wa Bulgaria kujitoa kufuatia majeraha ya bega.

Pambano hilo linalotarajiwa kuwa kali na la kuvutia litapigwa Oktoba 28 katika dimba la Cardiff ambapo mpaka sasa tiyari tiketi 70,000 zimeshauzwa.

Hili litakuwa pambano la kwanza la Antony Joshua tokea alipomtwanga Wladimir Klitschko katika dimba la Wembley mwezi April mwaka huu.

Antony Joshua alitakiwa kupambana na Kubrat Pulev lakini bondia huyo raia wa Bulgaria alipata majereha ya bega wakati akijiandaa na mchezo huo.

Takam mzaliwa wa Cameroon na anayeishi nchini Ufaransa ana miaka 36 na anatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Joshua.

Serikali kuwapunguzia muda wa masomo madaktari
Video: Lissu anyanyuka, Watanzania wanaokamatwa China madawa wafyekwa