Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini (TMDA), Adam Fimbo, ameitaka jamii kuwa na ufahamu katika utambuzi wa dawa halisi ama bandia hasa kwa dawa za aina ya antibiotiki.

Amesema kiashiria muhimu kwa dawa za aina hiyo katika kufahamu kama ni halisi ama bandia ni uwepo wa harufu ya dawa hizo kwenye mkojo wa mtumiaji.

“Kama hutasikia harufu ya dawa hiyo kwenye mkojo ujue hakuna dawa humo,” amesisitiza Fimbo.

Fimbo amesema hayo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku nne kwa Wakaguzi wapya 59 kutoka kanda nane za mamlaka hiyo yanayofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Amebainisha kuwa TMDA wamekuwa na utaratibu wa kuandaa mafunzo hayo mara kwa mara, ili kuwajengea Wakaguzi hao uwezo wa kuzuia mianya ya kuingiza dawa bandia ama zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu.

Fimbo ameongeza kuwa, kwa upande wa dawa za Wajawazito za kuongeza damu za Iron (Foric Acid) , lazima baada ya kutumia dawa hizo kinyesi cha mtumiaji kiwe cheusi kuashiria ni dawa sahihi.

Aidha amesema dawa zote zilizosajiliwa ama zilizokaguliwa na TMDA zinatakiwa kuwa na namba za Mamlaka hiyo za usajili, ili kuwahakikishia watumiaji ubora na viwango vilivyokusudiwa katika matumizi.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 9, 2021
Rais Samia afanya uteuzi