Mshambuliaji wa FC Barcelona Antoine Griezmann ameendelea kuwa sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa wanaowania kuifika na kuivunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote.

Rekodi hiyo katika timu ya taifa ya Ufaransa kwa sasa inashikwa na aliyewahi kuwa mshambuliaji na nahodha Thierry Henry aliyepachika mabao 51.

Griezmann anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaodhamiria kuifikia na kuivunja rekodi hiyo, baada ya kufunga dhidi ya Croatia, huku mwishoni mwa juma lililopita akifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Ujerumani.

Idadi hiyo imekuja baada ya jana kufunga bao la kwanza kwa Ufaransa dakika ya nane ya mchezo akisaidia taifa lake kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Mchezo huo uliokuwa wa kuvutia huku Croatia wakitawala zaidi kipindi cha pili na kuwezesha kusawazisha bao dakika ya 64 kupitia kwa Nikola Vlasic, lakini harakati hizo hazikuzaa matunda kwani Ufaransa walirudi na kufunga bao la ushindi kupitia kwa Kylian Mbappe.

Kylian Mbappe sasa ameifungia Ufaransa mabao 16 na kumfanya awe sawa na Franck Ribery na Laurent Blanc, huku Griezmann akiwa nyuma kwa goli moja, akitanguliwa na mshambuliaji wa zamani wa Les Bleus David Trezeguet.

Wafungaji Bora wa timu ya taifa ya Ufaransa wakati wote:

â—‰ Thierry Henry (51)

â—‰ Olivier Giroud (42)

â—‰ Michel Platini (41)

â—‰ David Trezeguet (34)

â—‰ Antoine Griezmann (33)

Watu 12 wafa kwa mafuriko Dar
G20 yarefusha muda wa mataifa masikini kulipa madeni