Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Antoine Griezmann anaonekana kuwa atacheza msimu wake wa mwisho akiwa na Atletico Madrid ya Hispania na msimu ujao atakuwa nyota anayefuata kuelekea Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS).

Mshambuliaji huyo hajawahi kufanya siri juu ya mapenzi yake kwa utamaduni wa Marekani, wala hamu yake ya siku moja kucheza MLS.

Siku hiyo sasa inaweza kuja mwaka ujao, kulingana na taarifa zinazosambaa Hispania kwa sasa.

Jarida la Sport, linasema Atletico inafahamu kuwa klabu kadhaa za MLS tayari zimewasiliana na mshindi huyo wa Kombe la Dunia na Ufaransa.

Atletico wanaripotiwa kuamini kwamba Griezmann anataka kuondoka katika mji mkuu wa Hispania mwishoni mwa msimu huu, huku fowadi huyo akisemekana kuwa anaonekana kupendelea kucheza ligi yenye presha ndogo.

Atletico, inasemekana kuwa tayari wanafikiria kuchukua Frederico Chiesa ili kuziba pengo la Griezmann.

Azam FC kumng'oa John Noble Tabora
Ntibanzonkiza, Mayele wabadili kanuni TPLB