Mshambuliaji Antoine Griezmann ameshinda kiatu cha dhahabu kwenye Michuano ya Euro mwaka huu baada ya kufunga magoli sita na kutoa pasi mbili zilizozaa mabao ndani ya dakika 555 alizocheza.

Cristiano Ronaldo na Olivier Giroud wamemaliza nafasi ya pili na ya tatu.

Hata hivyo, Griezmann (25) na timu yake ya Ufaransa jana walikuwa na huzuni kubwa baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ureno na amesema kwamba tuzo hiyo haina maana yoyote kwake kutokana na timu yake kukosa ubingwa dating i norge ambao wao ndio walikuwa waandaaji wa mashindano hayo.

Mchezaji huyo wa klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania, amekua  moja ya wachezaji mahiri kwenye michuano ya mwaka huu, lakini nafasi zake mbili alizopata kwenye mchezo wa jana hazikuweza kuzaa matunda. Griezmann amesema zawadi hiyo pengine ataisherehekea baadaye.

“Kuna ukatili na faraja kwa wakati mmoja,” Griezmann amesema. “Tumekuwa na wakati bora sana, lakini vile vile wakati wenye huzuni kubwa. Tunapaswa kujifunza. Lakini usiku wa leo (jana) tumejitahidi kwa kila namna na hatujutii kwa hilo. Ninajivunia kikosi chetu na kila mmoja wetu. Kilichobaki kwa sasa ni kupumzika na kuja na nguvu mpya.

“Safari hii tumeshindwa kufurukuta tofauti na ilivyokuwa dhidi ya Ujerumani. Kiukweli inauma sana. Tumepiga miamba, nilipata nafasi pia na ilibaki kidogo tu nifunge. Kipa akafanya kazi yake vyema. Inahuzunisha sana, lakini hakuna jinsi zaidi ya kujipanga na kurudi na nguvu mpya.”

Alipoulizwa kama anajivunia kushinda tuzo ya ufungaji bora, Griezmann alisema kamwe hawezi kuwa na furaha nayo kwa sasa hasa baada ya kuona timu yake ikipoteza na badala yake amesema muda huu akili yake yote ipo kwenye timu.

“Labda kwa baadaye ndiyo naweza kuihisi hii tuzo, lakini kwa sasa hapana. Lazima kwa pamoja wachezaji wote tuwe na huzuni. Napatwa na huzuni kubwa nikiwaangalia wachezaji wenzangu. Nilitaka kutoa mchango wangu kubakisha taji hili hapa. Lakini ndiyo hivyo imeshindikana hakuna namna tena.”

Zeben Hernandez: Azam FC Mpya Inakuja
Renato Sanches Mchezaji Bora Euro 2016