Meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte, amezipa kisogo fununu za kutomuhitaji tena kiungo kutoka nchini Hispania Cesc Fabregas katika kikosi chake, baada ya kupangua maswali ya waandishi wa habari mara baada ya mpambano uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya West Ham Utd.

Conte aliwashangaza mashabiki wengi wa The Blues waliokua wanaufuatilia mchezo huo uwanjani pamoja na runingani kufuatia maamuzi aliyoyachukua dhidi ya Fabregas ya kumuacha katika kikosi chak cha kwanza, jambo ambalo lilizua maswali mengi.

Mara baada ya mchezo huo, Conte alizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo huo, lakini aliulizwa kwa nini alichukua maamuzi ya kumuacha nje Fabregas ili hali inafahamika kiungo huyo amekua msaada mkubwa tangu alipokubali kujiunga na Chelsea mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea FC Barcelona.

Conte alijibu swali hilo kwa mkato kwa kusema ni maamuzi ya kawaida na haina maana kama Fabregas hana nafasi katika kikosi chake.

“Cesc ni mchezo wa Chelsea na ninaamini uwepo wake hapa una maana kubwa kwangu na watu wengine ambao wanahusika na Chelsea,” Alisema Conte

“Anapaswa kufahamu kwamba unapokua katika klabu kubwa kama Chelsea, unastahili kufahamu maamuzi ya mwisho yanatoka kwa meneja ambaye anajua nani anafaa kucheza katika mchezo gani na kwa wakati gani.

“Ni vizuri kuona suala hilo linaheshimiwa na sioni tatizo kuchukua maamuzi ya kumchezesha fulani na kumuacha mwingine, kwani naamini wachezjai wangu wote wana nafasi ya kucheza kila wakati. Alisisitiza Conte.

Kuachwa nje kwa Fabregas kumeibua taarifa nyingi mapema hii leo, ambapo miongoni mwa taarifa hizo inasemakana huenda kiungo huyo akaamuoa kuondoka kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwishoni mwa mwezi huu, kutokana na kuamini hana nafasi ya kucheza chini ya meneja huyo kutoka nchini Italia.

Rais wa Zambia atangazwa kushinda uchaguzi, wapinzani wang’aka
Video: Tofauti ya Hotel, Motel na Lodge