Bosi wa kikosi cha Chelsea Antonio Conte amejipanga kutumia silaha zake zote katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Man Utd, ambao umepangwa kuchezwa mwanzoni mwa juma lijalo.
Conte amethibitisha kupanga mipango hiyo, kwa kuamini mchezo huo utakua na vuta ni kuvute, kutokana na kila upande kuwa na matamanio ya kusonga mbele.
Conte ameviambia vyombo vya habari, haoni sababu ya kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake katika mchezo huo, kwa sababu hana cha kupoteza kwa kuhofia kuumia ama kuchoka.
Wachezaji kama Eden Hazard na Diego Costa ambao walikosa mchezo wa 16 bora ya kombe la FA dhidi ya Hull Wolves, wanatarajiwa kuungana na wenzao wa kikosi cha kwanza kama N’Golo Kante, Marcos Alonso, Thibaut Courtois na Gary Cahill.