Kocha wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amemwambia kocha wa Manchester United Jose Mourinho kwamba aangalie timu yake na aache kufuatilia masuala ya klabu ya Chelsea.

Kauli ya Antonio Conte inakuja baada ya Jose Mourinho kudai kwamba kuna makocha ambao wachezaji wao wakipata maejeraha huwa wanapiga sana kelele kauli ambayo ilionekana kama kijembe kwa Conte.

”Kila wakati Mourinho lazima azungumzie kile kinachoendelea Chelsea nadhani ni wakati anafaa kuzungumzia kikosi chake na ajitazame badala ya kutazama wenzake,” alisema Conte alipoulizwa kuhusu matamshi ya Mourinho ambayo hayakumlenga yeye moja kwa moja.

Conte amesema hawezi kuhatarisha afya za wachezaji wake na kwa kuwa wameumia kidogo atawaacha nje ya uwanja hadi pale watakapokuwa fiti kuanza kucheza.

Chelsea imeambulia alama moja tu katika michezo yao mitatu iliyopita katika msimu huu na Jumamosi hii wataikabili Watford huku Ngolo Kante,Victor Moses,Tiomoue Bakayoko na David Luiz wakiwa mashakani kuukosa mchezo huu.

UVCCM: Rushwa bado ni tatizo kubwa
Dkt. Ndugulile awaonya watumishi wa afya wenye lugha chafu