Baada ya uongozi wa Young Africans na kampni ya GSM kurejesha uhusiano uliokua njiani kuvunjia, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wameombwa kuendeleza umoja na mshikamano.

Rai hiyo kwa wanachama na mashabiki imetolewa na Afisa Uhamasihaji Antonio Nugaz, alipokua akieleza mipango na mikakati ya kuelekea kwenye mabadiliko ambayo mchakato wake wa awali utakamilishwa mwezi Mei.

Nugaz amesema mshikano wa uongozi na kampuni ya GSM uliodhihirishwa kupitia vyombo vya habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo mwanzoni mwa juma hili, unapaswa kuchukuliwa kama mfano wa kuwaweka pamoja Wanayanga kwa maslahi mapana ya klabu.

“Ni wakati wetu sasa wanachama,wapenzi na mashabiki wa Young Africans Sc kuwa pamoja na lengo letu liwe moja”

“Tushikamane kisawasawa kwa sababu hivi karibuni tunakwenda kwenye mabadiliko ya kweli na yenye tija kwa maslahi mapana ya Timu ya Wananchi.”

“Insha Allah Nina imani kubwa sana ndani ya Miaka 5 ijayo YOUNG AFRICANS  itakuwa miongoni mwa timu tano zenye uwezo (Kifedha,kisoka,kimfumo) na nguvu barani Afrika na za mfano wa KUIGWA kuliko timu yeyote Afrika Mashariki na Kati na kuanzisha

“Mwananchi Foundation” yenye uhalisia na mantiki halisi ya Timu ya Wananchi ili kurudisha kwa jamii kile kidogo kinachopatikana”

“Kikubwa ni Subra na imani na Uongozi chini Mwenyekiti Dkt Mshindo Msolla na Katibu Mkuu wetu Dkt David Ruhago na uwepo wa Brand Chapa Gsm kwenye kuchagiza mabadiliko ambao wao Gsm ndio wanayafadhili na ndio chachu ya kile tunachokilenga Young Africans”

“Shukran sana Sportpesa Mdhamini wetu mkuu , Ahsante sana Taifa Gas, Azam TV, Afya Drinking na Kongole Chapa Gsm Mdhamini, Muhisani na Mfadhili.”

Rwanda: Waziri afukuzwa, maambukizi ya Corona yaongezeka
Rais aongeza siku za Karantini nchi nzima Afrika Kusini