Kiungo Mshambuliaji ‘WINGA’ wa Manchester United, Antony amerejea England kutoka kwao Brazil na anatarajiwa kukutana na polisi kwa ajili ya tuhuma nyingi za unyanyasaji wa wanawake zinazomkabili.
Antony hajaichezea United tangu walipochapwa mabao 3-1 na Arsenal kwenye mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa mapema mwezi huu.
Aliondolewa kwenye kikosi cha Brazil kwa ajili ya mechi zao za kimataifa za Septemba kufuatia madai ya kwanza ya kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake Gabriela Cavallin.
Madai zaidi ya shambulio tangu wakati huo yametolewa na wanawake wengine wawili, Rayssa de Freitas na Ingrid Lana, matukio hayo yakidaiwa kutokea England na Brazil.
Imeelezwa kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 sasa amerejea England, lakini ataendelea kuwa likizo ya kutokuwapo na kikosi cha United.
Tayari aneshirikiana na polisi wa Brazil, ikiwa ni pamoja na mahojiano ya hiari Juni.
Hakujakuwa na mtu aliyekamatwa na hakuna mashtaka yaliyotolewa dhidi ya Antony, ambaye hapo awali alisema kuhusu madai hayo: “Nataka kusisitiza sina hatia kwa mambo ambayo nimekuwa nikishutumiwa.”