Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la James Msengi, mkazi wa Tabora anayekadiriwa kuwa na umri miaka 40 amenusurika kifo baada ya kujaribu kujiua kwa kujikata na kisu shingoni katika Tukio hilo limetokea kituo cha Msamvu mkoani Morogoro.

Majeruhi huyo, amelazwa katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ambapo amesema alikuwa akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Tabora na alipofika katika kituo hicho cha mabasi aliamua kutaka kujiua kwa ugumu wa maisha na kutokuwa na ajira.

Katibu wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Scholastika Ndunga amethibitisha kumpokea majeruhi akiwa katika hali mbaya na kutokwa na damu nyingi shingoni na kuanza kupatiwa matibabu ambapo kwa sasa anaendelea vizuri.

Shuhuda wa tukio hilo, mzee Ibrahim omary ambaye majeruhi alitumia kisu chake cha kuuzia miwa kujikata koromelo amesema, mtu huyo alifika katika eneo analofanyia biashara na kutaka auziwe muwa ambao haujamenywa na apewe kisu, lakini walishangaa baada ya kupewa kisu alianza kujichinja mwenyewe.

Kenya: Viongozi Azimio waidhinisha maamuzi kupinga matokeo
Hersi Said: Tutatetea mataji yetu Ligi Kuu, ASFC