Mfanyabiashara Leonard Kamili (31), jana alifikishwa mbele ya Haimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu akikabiliwa na shtaka la kumtishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwenye Mtandao.

Akisoma shtaka dhidi yake, Wakili wa Serikali, Diana Lukondo alisema kuwa mshatakiwa alituma ujumbe wa kumtishia Rais Magufuli Julai 17 akiwa jijini Dar es Salaam kupitia Mtandao wa WhatSapp huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa.

Alisema kuwa ujumbe huo wa vitisho ulisomeka, “Magu ajiandae tunaenda kupindua hadi Ikulu.” Alifafanaua kuwa mtuma ujumbe alikusudia kumtishia Rais Magufuli kupitia ujumbe huo.

Hata hivyo, Mshitakiwa alikana mashataka dhidi yake na upande wa Serikali uliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Mahakama hiyo ilimuachia Kamili kwa dhamana baada ya kutekeleza masharti yote ikiwa ni pamoja na kuwasilisha watu wawili watakaosaini dhamana ya shilingi milioni 5 kila mmoja. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Agosti 20 mwaka huu.

Magufuli apigilia Msumali Mbowe kutupiwa virago na NHC
Jaffo Asema Serikali Itaendelea Kugawa Maeneo Kwa Kuzingatia Katiba na Sheria