Beki wa Klabu ya Flamengo, Gustavo Henrique, hivi karibuni alilazimika kuondolewa uwanjani baada ya kuumia korodani na kuanza kuvuja damu.

Hii ilikuwa kwenye mchezo kati ya Flamengo na Corinthians ambao timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao matno kwa moja.

Tukio la kuumia mchezaji huyo lilitokea kipindi cha kwanza, baada ya beki huyo kugongana na mchezaji wa Corinthians.

Baada ya hapo damu zilionekana kuvuja kutoka kwenye bukta ya beki huyo na aliamua kutoka na kuvaa bukta nyingine na alipojaribu kuendelea kucheza alionekana kuwa na maumivu.

Kocha wa Flamengo, Domenec Torrent ilibidi amtoe beki huyo dakika sita kabla ya mapumziko na kwenda kupatiwa matatibu kwenye chumba cha kubadilishia nguo, lakini damu ziliendelea kutoka huku akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Dodoma Jiji wahamia Iringa
Serikali ya Nigeria yatangaza marufuku ya kutoka nje