Familia moja nchini Rwanda imejikuta katika majonzi ya muda mrefu baada ya binti yao kupooza kiakili na kimwili siku ya harusi yake hali iliyosabbaisha harusi kusitishwa na kumuwahisha hospitali.
Wakizungumza na Afrimax, familia ya Faina, mwenye umri wa miaka 38 kutoka Rwanda, ilisema kuwa aliondoka nyumbani kwenda mjini kutafuta kazi baada ya kushindwa kumaliza shule kwa kukosa karo ya Shule na alipopata kazi ya kuwa msaisizi wa ndani, alikuwa ndiye wa kutegemewa kiuchumi na familia hiyo.
Wamesema baadaye alikutana na mwanamume, na wakapendana hadi kupanga harusi yao, hivyo akarudi kijijini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho, na hapo ndipo mambo yakaanza kwenda mrama.
Baba yake Faina, alisema jambo lisilo la kawaida lilitokea siku ya harusi ambapo bibi harusi wa wakati huo akiwa na umri wa miaka 20, alianza kulalamika kuhisi mgonjwa.
“Alianza kuumwa na kichwa, akahisi kizunguzungu na akaanza kuwa na wazimu mitaani. Faina hakuweza kuzungumza na kutembea, hivyo akaanza kutambaa.” Harusi ikasitishwa, Faina akapelekwa hospitalini, akapata nafuu. Lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi, na miguu yake ikakunjana, hivyo alishindwa kutembea,” alisema baba yake.
Faina hutumia muda mwingi akiwa nyumbani kwa sababu hawezi kutembea, na familia yake sasa inaomba msaada wa kifedha ili kumnunulia kiti cha magurudumu.
Dada yake mkubwa, Alphonsine, alisema anashuku ni sabbat ya nguvu za giza zilizosababisha janga hilo, kwa kuwa Mchumba wa Faina alingoja kwa miaka mitatu, lakini baadaye alikata tamaa na kumuoa mwanamke mwingine na kujaliwa watoto watatu.