Mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Manyara ametajwa kuwa ‘HAKIMU’ wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho kati ya Young Africans dhidi ya Simba SC utakaochezwa Jumapili (Julai 25), Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Aragija ametajwa kuwa Mwamuzi wa mchezo huo akitarajia kusaidiwa na waamuzi wa pembeni Frednand Chacha kutoka Mwanza na Mohamed Mkono kutoka Tanga.

Arajiga anakabidhiwa jukumu hilo, huku akikumbukwa kwa maamuzi ya kuruhusu mpira wa adhabu kupigwa haraka haraka wakati wa mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC uliochezwa mjini Songea mkoani Ruvuma mwishoni mwa mwezi Juni.

Mpira huo wa adhabu ulizaa bao pekee na la ushindi kwa Simba SC, huku Mwamuzi huyo akilalamikiwa na baadhi ya wachezaji wa Azam FC kwa madai hakupaswa kuruhusu kitendo hicho.

CCM yampongeza mbunge Mabula kwa ziara yenye tija kwa wananchi
Naibu Waziri: TCRA, UCSAF kufikia agosti 16 muwe mmepata sululisho