Kiungo wa FC Barcelona Arda Turan amestaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Uturuki.
Turan mwenye umri wa miaka 30 ametumia ukurasa wake wa instagram kutangaza uwamuzi huo, baada ya siku tatu tangu afukuzwe kwenye kambi ya timu ya taifa na kocha Fatih Terim.
Turan alifukuzwa kambini baada ya kugombana na mwandishi wa habari wa gazeti la michezo la Milliyet, Bilal Mese wakiwa ndani ya ndege wakitokea Macedonia walipokua wamekwenda kucheza mchezo wa kirafiki ulioisha kwa sare ya bila kufungana.
Ndege ikiwa angani Turan alimvamia Mese na kumkaba koo lake na kumtolea lugha kali akidai kuwa mwandishi huyo mwenye miaka 70 alimtukana wakati wa fainali za Euro zilizofanyika mwaka jana nchini Ufaransa.
Turan ambaye alikuwa nahodha amevituhumu vyombo vya habari vya Uturuki vimekuwa vikimuandika vibaya.Vimekuwa vikiingilia maisha binafsi ya watu na kuandika habari za uzushi.