Kocha Mkuu wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Aristica Cioaba, ameweka wazi kuwa anakiamini kikosi chake kitakusanya pointi zote tatu kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo unaotarajia kuwa mkali na wa aina yake utafanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumatatu ijayo, ambapo Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 22 sawa na Simba iliyokileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa huku Mtibwa Sugar ikijikusanyia pointi 17 katika nafasi ya tano sawa na Singida United iliyojuu yake.

Cioaba amesema kuwa hawezi kuruhusu timu pinzani iharibu kazi yao nyumbani katika viunga vya Azam Complex, huku akikiri kazi haitakuwa rahisi kuibuka na ushindi.

“Kuhusu mechi yetu ijayo (Mtibwa Sugar), unaona kila mechi tunayocheza hapa Azam inakuwa ngumu timu zote pinzani zinataka kucheza vizuri dhidi ya Azam FC kila mmoja anahamasika, lakini wachezaji wanafahamu hii hali, nimewaona wamekuwa waangalifu wanapoingia kwenye mechi na kushinda mechi.

“Naiamini timu yangu kuwa mechi ijayo hapa Chamazi itakusanya pointi zote tatu, kwani sitaki kutoa nafasi hapa kwenye uwanja wangu kwa timu pinzani kuharibu kazi yetu…morali ipo juu kwa wachezaji, wamerudi wakitoka kwenye mchezo uliopita Njombe na wameshinda, wachezaji wanafuraha, siku hizi mbili za mazoezi wametulia,” alisema.

Idd Kajuna aitumia salamu Lipuli FC
Gambo awaahidi makubwa wakazi wa Kata ya Muriet