Timu ya New Castle United imeonesha nia ya kutaka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka.
Xhaka aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Arsenal kwa sasa hana nafasi ndani ya kikosi cha kwanza baada ya kutofautiana na mashabiki wa timu hiyo.
AC Milan nao pia hawapo mbali wanaiwinda saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 kwa sasa.
Kwa upande mwengine David Beckham ambaye ni mkufunzi wa timu ya Inter Miami ana matumaini ya kumsaini kiungo Mcroatia anayekipiga Real Madrid Luka Modric.
Beckham ambaye ni mchezaji wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya England kwa sasa yupo Inter Miami.
Beckham amekuwa akihusishwa kutaka kuwasaini mastaa wakubwa Ulaya kwenye kikosi chake cha Inter Miami ili kuongeza ushindani kwenye Ligi Kuu ya Marekani.