Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal), wameendelea na harakati za kukibomoa kikosi cha manbingwa wa soka nchini England Leicester city, kwa kuanza mazungumza na kumsajili kiungo mshambuliaji Riyad Mahrez.

Arsenal wameripotiwa kuanza mazungumzo ya usajili wa kiungo huyo kutoka nchini Algeria, ikiwa ni siku mbili zimepita ambapo ilielezwa walituma ofa ya Pauni milioni 20 kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji wa Leicester city, Jamie Vardy.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameona kuna umuhimu wa kufanya harakati za kuwasajili wachezaji hao wawili, kutokana na uhusiano mzuri waliouonyesha msimu uliopita, na kupelekea The Foxes kutwaa taji la ligi kuu ya England.

Hata hivyo huenda katika mazungumzo ya pande hizo mbili kuhusu usajili wa kiungo Mahrez, yakamuhusisha mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott kama sehemu ya uhamisho wake wa kujiunga na Leicester city.

Meneja wa The Foxes, Claudio Ranieri ameshindwa kuthibitisha kuhusu taarifa za usajili wa wachezaji hao wawili, na badala yake aliwataka waandishi wa habari kusubiri na kuona kama mpango huo utafanikiwa.

Mahrez, mwenye umri wa miaka 25, aliigharimu Leicester city kiasi cha Pauni 400,000 kama ada yake ya usajili mwezi Januari mwaka 2014, akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Le Havre.

TRA yameza rasmi mabilioni ya Rugemalira, yashinda kesi
Mjadala kuhusu wapinzani na Naibu Spika kuunguruma leo Bungeni