Kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere atakua nje ya kikosi cha klabu hiyo kwa muda wa majuma matatu, kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu ambayo yalimkosesha mchezo wa kuwania ngao ya jamii uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Chelsea.

Wilshere alianza kukabiliwa na majeraha hayo wakati kikosi cha Arsenal kilipokuwa kikijiandaa na mchezo wa ngao wa jamii.

Hata hivyo, kuumia kwake kumezua hofu kwa madaktari wa klabu ya Arsenal, kutokana na tatizo lililokua likimkabili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 miaka kadhaa iliyopita, hadi kufikia hatua ya kufanyiwa upasuaji.

Madaktari wa klabu hiyo wanahisi huenda Wilshere ameshutia sehemu ya kifundo cha mguu wake wa kulia ambayo ilimsababishia kufanyiwa upasuaji mwaka 2011, na kujikuta akikaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita.

Kufuatia taarifa hizo, Wilshere hatokua sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya England ambacho kitacheza mchezo wa kuwnai kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya, dhidi ya San Marino mnamo Septemba 5 na kisha kupambana na Uswiz siku tatu baadae.

Waziri Mwingine Wa Kikwete Aanguka
Hali Tete Kwa Mulumbu, Aanza Vibaya Norwich City