Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal) wameripotiwa kuanza maandalizi ya kumsaka mbadala wa Arsene Wenger.

Meneja huyo kutoka nchini Ufaransa atamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu, na tayari imeanza kudaiwa ana nafasi finyu ya kuongezewa mkataba mpya.

Gazeti la Daily Mirror limeandika kuwa, tayari majina manne ya mameneja ambao wanadhaniwa wanaweza kuimudu nafasi ya Wenger yameshawasilishwa katika meza ya bodi ya klabu hiyo.

Meneja wa klabu ya Borussia Dortmund Thomas Tuchel, anatajwa kuwa kinara katika orodha hiyo, akifuatiwa na mkuu wa benchi la ufundi wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC Max Allegri.

Pia lipo jina la meneja wa klabu ya AS Monaco Leonardo Jardim na Roger Schmidt wa Bayer Leverkusen.

Wenger amekua katika utawala wa benchi la Arsenal tangu mwaka 1996, na kwa sasa anahaha kusaka ubingwa wa England kwa zaidi ya miaka minane bila mafanikio.

Maalim Seif: Sioni sababu ya kuzungumza na Lipumba
Zitto Kabwe akesha bungeni, akihofia kukamatwa na polisi