Mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic, amesema alikua anawaniwa na klabu za Arsenal na Manchester City, kabla ya kufanya maamuzi ya kuelekea Old Trafford mwanzoni mwa mwezi Julai.

Zlatan amefichua siri hiyo ikiwa ni siku chache zimesalia kabla ya mpambano wa Man Utd na Man City ambao utaunguruma katika uwanja wa Old Trafford.

Amesema alikua katika mikakati ya kutafakari kujiunga na klabu ya Arsenal ama Man City kabla ya kupata uhakika wa kujiunga na Man Utd, lakini ujio wa Jose Mourinho ulimbadilisha mawazo na kuamua kuvaa jezi ya mashetani wekundu.

“Nilikaribia kujiunga na moja ya klabu mbili tofauti za nchini England, ambazo ni Arsenal na Manchester City.”Lakini ninashukuru jambo hilo halikutokea, kufuatia mipango niliyokua nimejiwekea kutimia.

“Mourinho alikua jibu sahihi kwangu katika kufanya maamuzi ya kuzikataa klabu za Arsenal na Man City, kwa sababu niliona bado kuna umuhimu wa kufanya nae kazi, baada ya kufanya hivyo tulipokua Inter Milan. Alisema Ibrahimovic

Ibrahimovic amekua na mwanzo mzuri tangu alipoanza kuitumikia klabu ya Man Utd mwanzoni mwa msimu huu, na ameanza kutabiriwa huenda akafanya vyema katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Man City.

MILLIONI 30 KUGOMBANIWA NA NCHI TANO EAST AFRIKA NDANI YA MAISHA PLUS
Cristiano Ronaldo: Zidane Ni Ufunguo Wa Mafanikio Ya Real Madrid