Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech aliokoa mara mbili mipira ya hatari iliyokuwa ikielekea langoni mwake na kuisaidia timu yake kupata alama moja katika mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool.

Katika mchezo huo mikwaju miwili ya Philippe Coutinho ililenga mwamba huku kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey akikataliwa goli alilofunga kipindi cha kwanza kutokana na kuwa katika mstari wa kuotea.

Cech aliokoa kwa mara nyingine mkwaju wa karibu wa Christian Benteke na kuucheza tena kwa umahiri mpira uliopigwa na Coutinho uliokuwa unaelekea kwenye nyavu.

Juhudi za Alexis Sanchez ziliishia kulenga mwamba kabla ya mlinda mlango wa Liverpool Simon Mignolet kuokoa mkwaju wa Olivier Giroud.

Hata hivyo, Arsenal ilifanikiwa kupata bao lililofungwa na Aaron Ramsey dakika ya tisa, lakini muamuzi wa pembeni akalikataa kwa sababu alikuwa ameotea.

Kipa Petr Cech aliokoa michomo miwili ya hatari ya Christian Benteke na Philippe Coutinho kipindi cha kwanza, huku Olivier Giroud naye akikosa bao la wazi.

Liverpool wanamaliza mechi ya tatu bila kufungwa bao baada ya kushinda 1-0 mara mbili dhidi ya Stoke City na Bournemouth katika mechi zake mbili za awali za Ligi Kuu.

Wakenya Wafanya Kweli Mjini Beijing
Dk. Shein Amkana Maalim Seif, Adai ZEC Iko Sawa Na CCM Itashinda