Klabu ya Arsenal imeanza vyema michuano ya Europa League baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Colgne katika mchezo wa kundi ‘H’ uliopigwa katika dimba la Emirates.
Nje ya uwanja wa Emirates msongamano mkubwa wa watu uliufanya mchezo kuchelewa kwa lisaa lakini baadae ulipigwa huku Colgne wakitangulia kupata bao kupitia Jhon Cordoba dakika ya 9.
Dakika ya 49 baada ya kipindi cha pili kuanza Sead Kolasinac wa Arsenal alisawazisha kabla ya Alexis Sanchez kufunga bao la pili dakika ya 67 huku Hector Berlin akiongeza bao la tatu na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Arsenal kushinda mabao 3-1.
-
Isco kubaki Santiago Bernabeu mpaka 2022
-
Paul Pogba huenda akawa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi
-
Video: Man City, Real Madrid zang’ara, Liverpool yabanwa
Katika mchezo mwingine Everton wameanza vibaya michuano ya Europa baada ya kufungwa mabao 3-0 na Atlanta, huku Villareal wakiipiga Fc Astana bao 3 kwa 1.
Andre Silva aliifungia Ac Millan hat-trick wakati wakiichapa Austria Vienna bao 5 kwa 1, huku Suso na Calhanoglu wakiipatia Ac Millan mabao mengine na lile la Austria Vienna likiwekwa kimiani na Borkavic.