Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Arsenal, Olivier Giroud, usiku wa kuamkia hii leo huenda alikosa usinginzi kama alikua anafuatilia mitandao ya kijamii.

Giroud, alishindwa kumaliza mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi ambapo Arsenal walikua ugenini wakipambana na Dynamo Zagreb, baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia mchezo wa hovyo aliouonyesha dhidi ya beki wa timu mwenyeji.

Mshambuliaji huyo aliadhibiwa kwa kadi ya pili ya njano iliyozaa nyekundu katika dakika ya 40, ambapo tayari Arsenal walikua nyuma kwa bao moja.

Kutokana na hali hiyo, mashabiki wa The Gunners walionyesha kuhamaki na kuanza kumtusi Giroud, kupitia mitandao ya kijamii na wengine walidiriki kumuita msaliti ambaye alikua chanzo cha timu yao kupoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi.

Hata hivyo huenda hasira za mashabiki wa Arsenal zilitokana na chuki waliyonayo kwa mshambuliaji huyo, ambaye mara kadhaa amekua akinyooshewa vidole kwa kuambiwa hatoshi katika harakati za kuisaidia klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London kufikia malengo yake.

Katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo, The Gunners walikubali kichapo cha bakora mbili kwa moja, ambapo mabao ya wenyeji Dynamo Zagreb yalipachikwa wavuni na Josip Pivaric pamoja na Domagoj Antolic huku bao la kujipoza la Arsenal likifungwa na Theo Walcott.

Kutokana na matokeo hayo, msimamo wa kundi la sita unaonyesha Arsenal wapo katika nafasi ya tatu wakifuatiwa na Olympiakos ambao pia walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya mabingwa wa soka nchini Ujerumani, FC Bayern Munich.

Michezo mingine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi iliyochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Champions League – Group E

Bayer Leverkusen 4 – 1 BATE Borisov

FTRoma 1 – 1 Barcelona

 

Champions League – Group G

Chelsea 4 – 0 Maccabi Tel Aviv

Dynamo Kyiv 2 – 2 FC Porto

 

Champions League – Group H

Gent 1 – 1 Lyon

Valencia 2 – 3 Zenit St. Petersburg

Magufuli Afunika Kigoma, Angalia Video
Shabiki Nguli Wa Brazil Afariki Dunia