Klabu ya Arsenal inafanya mazungumzo na mchezaji wa Chelsea raia wa Ujerumani, Kai Havertz kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili la joto.

Arsenal wanataka kuwasilisha ofa kwa klabu ya Chelsea kwa ajili ya kumnunua kiungo huyo wa kijerumani ambaye amekua hana msimu mzuri hivi na mwenyewe anataka kuondoka ndani ya timu hiyo.

Washikabunduki hao wa London wanataka kuwasilisha dau mezani kwa ajili ya Havertz pamoja na kiungo wa klabu ya West Ham United ambaye wamekua wakimfukuzia kwa muda mrefu, Declan Rice ili kuboresha timu yao kuelekea msimu ujao.

Havertz alikua akihitajika na klabu ya Real Madrid, lakini hadi sasa inaonekana wababe hao wa soka nchini Hispania wamejitoa katika mbio hizo, huku Arsenal sasa wakionesha nia ya dhati ya kumchukua kiungo huyo.

Arsenal wanataka kuboresha timu yao zaidi baada ya kuwa na msimu mzuri wa 2022/23 licha ya kukosa ubingwa wakiamini kama wataboresha timu yao na wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi msimu ujao na hata kubeba ubingwa.

Simba SC kumshusha Bongo Makabi Lilepo
Wabunge wasusia bajeti ya Waziri wa Fedha