Klabu ya Arsenal yafurahishwa na kiwango cha uchezaji wa kiungo mshambuliaji ambaye ni raia wa Misri, Mohamed Elneny (25 ) na kumuongezea mkataba wa kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu.
Elneny alijiunga na Arsenal Uswisi kwenye klabu ya Basel mwezi Januari, 2016 na tangu kujiunga na timu hiyo amefanikiwa kuichezea michezo 65.
Hata hivyo klabu hiyo haijaweka wazi ni mkataba wa muda gani wamempa kiungo huyo kutoka miamba ya soka Afrika, nchini Misri.
Aidha, Mchezaji huyo anatarajia kuwa sehemu ya kikosi cha Misri kitakacho shiriki fainali za kombe la dunia mwezi juni, nchini Urusi na kuisaidia nchi yake kufika mbali katika mashindano hayo.
“Rasmi tutakuwa pamoja kwa muda mrefu, kwa lengo la kutimiza kile tulicho kianzisha,na kuiweka Arsenal kwenye nafasi inayo stahili Ulaya na duniani kote’’ ameandika Elneny kwenye Akaunti yake ya mtandao wa Twitter.
Mchezaji huyo ni moja kati ya wachezaji wachache walioanzia kucheza ligi za barani Afrika kabla ya kwenda barani Ulaya, Kiungo huyo alikuwa akiichezea timu ya El Mokawloon inayoshiriki ligi kuu ya nchini Misri.