Kiungo Santi Cazorla wa klabu ya soka ya Arsenal na timu ya taifa ya Hispania ameumia na sasa anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi minne kocha Arsene Wenger amethibitisha.

Wenger anasema Cazorla aliumia goti na kwamba alifanyiwa scan Ijumaa hii na kugundulika atakua nje ya uwanja hadi mwezi machi mwakani.

Santi Cazorla aliumia katika mechi ya sare dhidi ya Norwich wiki iliyopita na kulazimika kucheza hivyo hivyo hadi mwisho wa mchezo huku kocha Arsene Wenger akisema Cazorla alimaliza mchezo huo akiwa na mguu mmoja.

Taarifa hizi ni mbaya na zinaumiza kwa mashabiki na benchi la ufundi la Arsenal kutokana na kuongezeka kwa idadi kubwa ya majeruhi ya wachezaji muhimu katika kikosi cha kwanza.

Mchezaji huyo anaungana na wengine kama Francis Coquelin, Jack Wilshere, Theo Walcott ambao wote ni wa kikosi cha kwanza na kumuacha Wenger akiwa na Mathew Flamini na Aaron Ramsey kuziba nafasi ya kiungo baada ya nahodha Mikel Arteta pia kuwa majeruhi, sanjari na Alexis Sanchez huku wakikabiliwa na mechi muhimu wanayohitaji ushindi ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Olympiakos Pireus Jumanne hii.

Arsenal iko katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini England nyuma ya vinara Leceister baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Sunderland wikend hii lakini wanahitaji fomu kama hii Jumanne katika usiku wa UEFA.

Pale Uwanja Wa Soka Unapogeuka Msitu Wa Vita
Mbeya City Yaanika Majina Ya Waliowasajili Dirisha Dogo