Kuelekea katika mchezo dhidi ya Barcelona, Wenger amesema: “Ni vigumu sana kushindana nao hasa ukizingatia uwepo wa washambuliaji wao watatu machachari (Messi, Neymar na Suarez), lakini lolote linaweza kutokea,” alisema.

“Inawezekana, kwa sababu baadhi ya vilabu vimefanikiwa kufanya hivyo, Bayern Munich wamefanya hivyo, lakini hupaswi kuwa na majeruhi katika kikosi chako.”

Arsenal Arsene Wenger amewaasa vijana wake kuongeza ari ya pale watakapovaana na Southampton leo usiku baada ya timu hiyo kupokea kipigo kitakatifu cha mabao 4-0, mchezo uliochezwa kunako dimba la St Mary’s siku ya Boxing Day.

‘The Gunners’ wana matumaini makubwa sana hasa kutokana na kurejea kwa Alexis Sanchez, na Francis Coquelin ambao walikuwa wakisumbuliwa na majeraha yaliyowaweka nje kwa muda wa miezi miwili. Sanchez alirudi kwa kishindo baada ya kufunga goli la ushindi katika ushindi wa mabao 2-1 ambao Arsenal waliupata dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa kombe la FA Jumamosi iliyopita.

“Wale vijana (Southampton) walitupa wakati mgumu sana katika mchezo uliopita na tunatakiwa kuhakikisha tunapambana kweli kweli,” Wenger aliwaambia wanahabari.

“Ujumbe wangu kwa sasa ni huu, tunacheza katika uwanja wa nyumbani na tunataka  kucheza kwa kiwango cha juu kutona na ari tuliyonayo hasa tunapokuwa katika uwanja wa nyumbani.”

Friends Rangers Wapiga Hesabu Za Kuwafuata Ruvu Shooting
Waliosajiliwa Siku Ya Mwisho Dirisha Dogo 2016