Beki kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Arsenal, Per Mertesacker  atakuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa, kufuatia maumivu wa goti aliyoyapata katika kipindi hiki cha kujiandaa na msimu wa 2016/17 ambao utaanza rasmi mwezi ujao.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kumkosa beki huyo alipozungumza na waandishi wa habari nchini Marekani ambapo The Gunners wamekwenda kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya msimu mpya.

Hata hivyo Wenger hakusema ni muda gani utamchukua Mertesacker  kuuguza majeraha yake, zaidi ya kusisitiza beki huyo mwenye umri wa miaka 31 atashindwa kucheza kwa miezi kadhaa.

Beki huyo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2014, alicheza mchezo wa kirafiki wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Lens ambao walilazimishwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Kuumia kwa Mertesacker, kunaifanya Arsenal kuendelea kuwakosa wachezaji wake muhimu wanaocheza nafasi ya ulinzi, ambapo tayari imeshathibitika Laurent Koscielny pamoja na Gabriel hawapo katika mchakato wa maandalizi ya kikosi hicho kwa sasa.

Gabriel anasumbuliwa na tonsillitis (Mafindofindo), Koscielny bado yupo katika mapumziko baada ya kumaliza majukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa kwenye fainali za Euro 2016.

Calum Chambers ni beki pekee aliyesalia kwenye kikosi cha Arsenal ambaye yupo fit.

West Ham Utd Wakaribia Kunasa Kinda La Argentina
Tajiri Wa Inter Milan Amalizana Na Roberto Mancini