Mechi za kuhitimisha hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zinachezwa leo barani humo, macho na masikio ya wengi yakiwa kwa Arsenal.

Arsenal leo watakuwa wageni wa Olympiakos  katika mchezo wa Kundi F Uwanja wa Georgios Karaiskakis wakihitaji lazima kushinda ili kwenda hatua ya mtoano.
Kwa sasa Arsenal ina pointi sita katika nafasi ya tatu, nyuma ya Olympiakos wenye pointi tisa na Bayern Munich pointi 12.

Chelsea watakuwa wenyeji wa FC Porto Uwanja wa Stamford Bridge katika mchezo ambao The Blues watahitaji japo sare tu kujihakikishia kusonga mbele.

Mechi nyingine za leo ni kati ya Valencia CF na Lyon, Roma na BATE Borisov, KAA Gent na Zenit St Petersburg, Dynamo Kyiv na Maccabi Tel Aviv na Kiev Olympic, Dinamo Zagreb na Bayern Munich na Bayer 04 Leverkusen na Barcelona.

Shule Binafsi Zatakiwa Kuwasilisha Ongezeko La Ada
TP Mazembe Na Etoile du Sahel Kupambana February 2016