Baada ya kubugia kisago cha mabao manne kwa matatu kutoka kwa majogoo wa jiji Liverpool, meneja wa Arsenal (Arsene Wenger) amejipoza kwa kuamini safu ya ulinzi ambayo aliitumia jana haikua chaguo sahihi.

Wenger amesema wachezaji aliowatumia katika nafasi hiyo hawakuwa na uzoefu wa kutosha kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya timu pinzani, jambo ambalo lilikua chanzo cha kukubali kufungwa mabao manne.

Amesema kukosekana kwa wachezaji wake ambao siku zote wamekua wakiitumikia nafasi hiyo, ilikua pigo kubwa sana, na hadhani kosa kama hilo litajiridia tena katika michezo inayofuata.

“Tulikosa ujuzi wa wachezaji wenye uzoefu na michezo ya ligi, lakini naamini mambo yatakaa sawa katika michezo inayofuata”

“Ni vigumu kumtumia mara moja mchezaji anaetoka katika fainali kubwa kama za Euro, hivyo wanahitaji mapumziko na kujiandaa vya kutosha.”

“Liverpool walifanya kazi nzuri, walituzidi kwa dakika 15 na wakatimiza malengo yao. Lakini hata wachezaji wangu walijitahidi lakini haikua bahati yetu kusawazisha. Alisema Wenger alipohojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza (BBC).

Katika mchezo wa jana mzee huyo kutoka nchini Ufaransa alimtumia Rob Holding na Calum Chambers kama walinzi wa kati, badala ya Laurent Koscielny (Hakuwa Fit) na Per Mertesacker (Majeruhi).

Mabao ya Liverpool katika mchezo huo yalifungwa na Philip Coutinho (45+1, 56), Adam Lallana (49) na Sadio Mane (63) huku ya Arsenal yakitumbukizwa kambani na Theo Walcott (31), Alex Oxlade-Chamberlain (64) na Calum Chambers (75).

Mchezo ujao wa ligi ya England, Arsenal watapambana na mabingwa watetezi Leicester City kwenye uwanja wa King Power.

Agosti 14 Haikua Siku Nzuri Kwa Petr Cech
Pep Guardiola Kumuuza Joe Hart?