Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema licha ya sare ya 2-2 dhidi ya Fulham iliyoku wa pungufu lakini anaamini kikosi chake kilipambana na kilikuwa bora mara kumi zaidi ya msimu uliopita.

Katika mdhezo huo uliopigwa juzi Jumamosi (Agosti 26) Arsenal iliyokuwa nyumbani iliamini imemaliza kazi baada ya mabao ya Bukayo Saka dakika ya 70 na Eddie Nketiah dakika 72 na kuongoza kwa mabao 2-1 lakini mambo yalitibuka baadae.

Licha ya Calvin Bassey kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 83 lakini Fulham walitutumka na Joao Palhinha kuchomoa bao hilo dakika ya 87 na kuzima ndoto za Arsenal kuondoka na alama tatu.

Tuliongoza kwa mabao 2-1 na ilipaswa kulilinda kwa iwezo wetu wote, huwezi kuruhusu bao baada ya kila kitu tulichofanya.

“Tulipaswa kufunga mabao tano, sita mpaka saba. Kama ukifananisha msimu huu na uliopita, tulikuwa bora mara 10 zaidi ya msimu uliopita,” alisema Arteta nahodha wa zamari wa timu hiyo.

Arsenal iliyomaliza ya pili msimu uliopita, iliruhusu bao dakika ya kwanza lakini Arteta alionekana kuhimili hali hiyo na kuweka mipango yake sawa sawa.

“Unapofaya makosa katika dakika ya kwanza kama vile tulivyofanya na kumpa bao mpinzani, mechi inakuwa ngumu zaidi. “Tulijaríbu kujibu mapigo mapema na tulitengeneza nafasi lakini hatukufanikiwa lolote. Tuliutawala mchezo kwa muda wote lakini hatukufunga bao,” alisema Arteta.

Hata hivyo, Arteta alinufaika na mabadiliko ya kuwaingiza Nketiah na Fabio Vieira kipindí cha pili ambao walimfurahisha Arteta na kukiri ulikuwa uamuzi sahihi kuwaíngiza vijana wake hao.

“Mabadiliko yalileta tofauti kubwa sana uwanjani na matokeo bora zaidi. Nimependa maamuzi na kujiamini kwao na kuibadili kabisa timu iliyokuwa ikipambana maradufu zaidi,” alisema raia huyo wa Hispania.

Makala: Huba la Grace chanzo anguko la Mugabe Kisiasa?
Rais Samia kuzindua jengo Umoja wa Posta Afrika