Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amewaomba wachezaji wake, hasa waandamizi kama Auba na Lacanyavu, wainusuru klabu yao kwenye aibu inayowaandama.

Arsenal wameshachezaechi mbili za ligi na kupoteza zote…bila kufunga hata bao moja.

Hii ni rekodi mbaya zaidi katika historia ya miaka 118 ya klabu hiyo.

Hata hivyo hii ni mara ya tatu kwa Arsenal kupoteza mechi mbili za kwanza za msimu, japo mara mbili za kwanza angalau walipata bao au mabao.

Mara ya kwanza ilikuwa msimu wa 1992/93 ambapo walipoteza mechi tatu mfululizo.

Kichapo cha nyumbani cha 4-2 kutoka kwa Norwich kilifuatana na kichapo kingine cha 1-0 kutoka kwa Blackburn na kingine cha 2-0 ugenini kwa Liverpool.

Mara pili ilikuwa msimu wa 2018/19 chini ya kocha Unai Emery.

Mechi ya kwanza walifungwa 3-0 na Manchester City, halafu wakafungwa 3-2 na Chelsea.

Mechi inayofuata ni dhidi ya Manchester City dimbani Etihad.

Hapo ndipo Arteta anaponusa harufu ya damu na kuwaomba wachezaji wake waandamizi wajitoe kwa.ajili ya timu kuepuka aibu inayoweza kutokea.

Mechi iliyopita Manchester City alimpa mtu mkono na ukizongatia Arsenal hawama rekodi nzuri kwenye uwanja huo.

Tuisila Kisinda atambulishwa rasmi RS Berkane
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 28, 2021