Baada ya kuambulia sare ya 0-0, Meneja wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amekubali kuwa kikosi chake hakikustahili kushinda dhidi ya Brighton and Hove Albion, ambao walikua nyumbani Amex Stadium, Jumamosi (Oktoba 02).
Arteta ametoa mtazamo huo baada ya kuona madhaifu ya kikosi chake kwenye mchezo huo ambao ni dhahir Arsenal ilikaribia kuondoka na ushindi kufuatia nahodha na mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang kugongesha mwamba na Emile Smith-Rowe kukaribia kufunga kipindi cha pili.
Meneja huyo kutoka nchini Hispania amesema: “Ninachofikiria ni namna tulivyocheza,”
“Hatukufanya maamuzi sahihi, kila wakati tulishindwa kuendana na presha ya mchezo na hatukushambulia kwa kasi.”
“Nafasi ya Aubameyang pengine ndio ilikuwa ya wazi zaidi ya kuweza kufunga katika kipindi cha kwanza, na hatukuwa na bahati ya kufunga.
“Sidhani kama tulistahili kushinda mchezo huu, tunatakiwa kushukuru kwa matokeo ya sare kama kiwango kizuri zaidi tulichocheza na hivyo tunahitaji kuimarika zaidi.”
Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kufikisha alama 10, zinazowaweka kwenye nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.