Mabingwa wa Kombe la FA na Ngao ya Jamii nchini England Arsenal FC, wapo mbioni kumsajili kwa mara ya pili kiungo mshambuliaji kutoka kwa mabingwa wa Hispania Real Madrid Dani Ceballos.
Mchezaji huyo alicheza Arsenal kwa mopo msimu uliopita akitokea Real Madrid, na alionyesha kiwango cha haliya juu, na kuisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa FA chini ya meneja Mikael Arteta.
Kiungo huyo ambaye hakua na mwanzo mzuri wa msimu chini ya kocha Arteta, alionesha kiwango kizuri na cha kuridhisha baada ya mapumziko ya Corona kumalizika.
Wakati Arsenal wakipanga mikakati ya kumsajili tena, Ceballos nae ameonesha kuwa anatamani kurejea kaskazini mwa jijini London kuendeleza makali yake, kwa kuweka video yake kwenye ukurasa wake wa Instagram akiangalia na kushangilia ushindi wa Arsenal shidi ya Liverpool katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
Arteta amesema ameongea na kiungo huyo na amemthibitishia kwamba, anataka kurejea Arsenal.
“Tumekua na mazungumzo na Dani, yeye anajua nnachofikiria kuhusu yeye. Nae amekua wazi kwangu kuwa anataka kubaki Arsenal”, alisema Arteta.
Ripoti kutoka jiji la Madrid zinaarifu kuwa Real Madrid wapo tayari kumuachia kiungo huyo kwa mkopo tena katika msimu wa 2020/21.
Ceballos anaamini kuwa ndani ya kikosi cha Arsenal atapata nafasi ya kucheza michezo mingin kuliko akiwa Real Madrid, na lengo lake ni kucheza michezo mingi kadri iwezekanavyo ili kulinda nafasi yake ndani ya timu ya taifa ya Hispania.