Mwanamke Marry Mushi ameuawa kwa kukatwa na shoka na mumewe, Moses Pollangyo ambaye ni muimba kwaya.

Tukio hilo lililowahuzisha wengi na kubadilisha sura ya sikukuu ya Noel, limetokea Jana katika Kijiji cha Kilinga.

Imeelezwa kuwa mwanaume huyo alichukizwa na kitendo cha mkewe kumpikia chai badala ya vyakula maarufu kwaajili ya sikukuu.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni wiki tatu tangu marehemu aanze kuishi na mtuhumiwa huyo Kama mke na mume.

Kwa upande wa Baba wa mtuhumiwa, Latiaeli Samson Pallangyo amesema hakukuwa na ugomvi wowote na walitegemea kusherekea siku ya Krismasi vizuri Mara baada ya marehemu kuwapikia chai.

Wasudan washerehekea Krismasi baada ya miaka 70
Papa Francis atuma ujumbe wa pekee kwenye ibada ya Krismas