Klabu ya Namungo FC sasa ni rasmi inakamilisha ratiba tu kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika zamani ikifahamika kama kombe la washindi baada ya kucheza michezo minne ikiwa haijashinda mchezo wowote na wala haijatoa walau sare.

Namungo FC wamepoteza michezo yote minne na hali yao ni rahisi kuielezea kuwa michuano iliwaelemea kiasi. Timu haijashinda mchezo wowote nyumbani ama ugenini lakini bahati mbaya kwao hata kufunga goli kwenye hatua hii hawajawahi ila wao wameruhusu magoli matano.

Wana mechi 2 mkononi dhidi ya Pyramids na dhidi ya Raja Casablanca! Watacheza na Raja nyumbani na watacheza na Pyramids ugenini lakini bahati mbaya hata wakishinda michezo hiyo haitakua suluhu kwao.

Kiuchezaji hawajawa dhaifu kiwanjani. Wamekuwa na mchezo mzuri usio na mashaka kuanzia kule nchini Morocco walicheza vyema kabisa shida ikawa kwenye makosa madogo madogo ambayo mara zote ndio huharibu taswira nzima ya michezo yao.

Timu inafanya build-up nzuri sana ya mashambulizi kutoka nyuma kwenda mbele na inapiga pasi za uhakika sana lakini usahihi wao wa matendo mara zote umeathiriwa na idadi yao kwenye eneo la wisho anapocheza Stephen Sey! Ametelekezwa sana kwenye eneo lake la kucheza.

Analazimika kuwasubiri sana wenzie wasogee juu hivyo kujikuta akipoteza mashambulizi. Wakati mwingine timu nzima haibadiliki kiuchezaji inapovuka msitari wa katikati ya kiwanja. Hawaongezi kasi, ubunifu na utulivu badala yake wanaenda taratibu na kuwasaidia wapinzani kurudi kwenye maeneo yao ya msingi ya kurudishia umiliki wa mpira.

Ubora wa mchezaji mmoja mmoja wa Namungo na ubora wa kikosi pia vinawahukumu Namungo!. Haijafanya uwekezaji mkubwa mizania ya Pyramids ambao mchezaji kama Eric Danga, Islam Fathi na Ahmed El Shenawy ni daraja la juu kabisa barani Afrika.

Hata kwa Raja wamefanya uwekezaji mkubwa kuliko Namungo na Nkana wao wana wachezaji wengi waliokwishakupata ukomavu wa namna ya kucheza michuano hii kuliko Namungo. Mtazame yule Duke Abuya, Harrison Chisala, Kampamba, Fred Tshimenga, Allan Chibwe n.k

Kama nchi, hatuwadai chochote Namungo!. Wamefanya kila kitu kwenye kiwango chao.

Wasalaam!

@nazareth_upete

Ujenzi bomba la mafuta fursa kwa Tanzania
Aweso akiri miradi ya maji kutokutoa maji, awaonya Wakandarasi, Wahandisi