Wapinzani wa Simba SC kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ASEC Mimosas, wameanza safari ya kuelekea Jijini Dar es salaam-Tanzania, tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi.

Simba SC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa ‘Kundi D’ siku ya Jumapili (Februari 13), utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye klabu ya ASEC Mimosas, kikosi cha klabu hiyo kimeanza safari leo asubuhi kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia.

Kikosi cha ASEC Mimosas kinatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam leo mchana, tayari kwa mchezo dhidi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

‘Kundi D’ la Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika lina timu za Simba SC (Tanzania), ASEC Mimosas (Ivory Coast), RS Berkane (Morocco) na US Gendermarie (Niger).

Magazeti manne yafunguliwa
Kesi ya Mbowe na wenzake kuunguruma tena Februari 14