Kikosi cha KMC FC kesho Jumatano (Desemba 15) kitashuka Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa michuano ya kombe la Azam Sports Federation ASFC dhidi ya Majimaji ya mkoani Ruvuma utakaopigwa saa 10:00 jioni.
Kikosi hicho cha Manispaa ya Kinondoni kimefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kiko tayari kwa mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kama Timu inakwenda kupata ushindi na hivyo kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
KMC FC inafanya maandalizi ya mchezo huo kwa kuzingatia kuwa michuano hiyo ipo katika hali ya mtoano na kwamba mkakati wa Timu ni kuhakikisha kuwa inaendelea kusonga mbele hadi hatua ya fainali na hivyo kuchukua kombe hilo.
Tunakwenda kwenye michuano ya ASFC ambayo kimsingi tunajua kuwa inaushindani mkubwa na ipo katika hali ya mtoano, kwamba ukifungwa ndio unakuwa umemaliza safari ya kusonga mbele, lakini pia Majimaji ni Timu nzuri na wao tunafahamu wanahitaji kufanya vizuri, hivyo tunakwenda kupambana uwanjani ili kupata ushindi.
“Hali ya kikosi iko vizuri kwa maana ya morali za wachezaji zipo juu, kila mmoja anahitaji Timu ifanye vizuri kwenye michuano hiyo kwa sababu tunamalengo makubwa ambayo ni kuchukua kombe hilo,kitu ambacho tunafahamu kinawezekana kwa sababu ipo ndani ya uwezo wetu”.
Imetolewa leo Disemba 14
Na Christina Mwagala
Ofisa Habari na Mawasiliano KMC FC