Mchezaji wa klabu ya Simba Erasto Edward Nyoni ameahidi kugawa tiketi 50 kwa mashabiki wa soka mjini Songea Mkoani Ruvuma, kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Azam FC, utakaochezwa Jumamosi (Juni 26), Uwanja wa Majimaji.

Nyoni ametangaza dhamira hiyo ili kuonesha upendo kwa mashabiki wake na kuwathamini ndugu zake wa mkoani Ruvuma, ambapo ndipo alikozaliwa.

Tayari Simba SC imeshawasili mjinni Songea Mkoani Ruvuma kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na vuta ni kuvute, kufuatia kiwango cha wapinzani wao Azam FC kwa sasa.

Nayo Azam FC imefika mjini Songea leo mchana ikitokea jijini Dar es salaam.

Simba SC ilitinga hatua ya Nusu Fainali ya ‘ASFC’ baada ya kuifunga Dododma mabao 3-1, huku Azam FC wakiivurumisha nje Rhino Ranger ya Tabora mabao 2-1.

Nusu fainali nyingine ya michuano hiyo itachezwa mjini Tabora kwenye Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi Ijumaa (Juni 25) kati ya Young Africans dhidi ya Biashara United Mara.

Mingange: Simba itawapigeni sana 4, 4
RC Makalla awahimiza watumishi kukopa, kuanzisha miradi