Julai 4, 2007, Joseph Christian Chestnut alishinda shindano la 92 la kila mwaka liitwalo “Nathan’s Hot Dog Eating” lililofanyika jijini New York nchni Marekani, akimshindwa Bingwa mtetezi mara sita Takeru “Tsunami” Kobayashi, kwa kula ‘Hot dogs buns’ 66 ndani ya dakika 12.
Mwaka uliofuata (2008), Chestnut pia alifanikiwa kutetea taji lake kwa kushinda taji hilo baada ya kula tena ‘Hot Dogs Buns’ tano zaidi juu ya Kobayashi aliyeteketeza ‘Hot dogs buns’ 59 ndani ya dakika kumi.
Julai 4, 2009, Chestnut akamshinda tena Kobayashi na kuweka rekodi ya dunia baada ya kula ‘Hot Dogs Buns’ 68 na kushinda taji lake la tatu mfululizo, na Julai 4, 2010 pia Chestnut alirudi nyumbani na ushindi wake wa 4 mfululizo wa Mustard akila ‘Hot Dogs Buns’ 54.
Shindano la 2010 lilikuwa la ushindi wa jumla kwa Chestnut, kwani Kobayashi hakushindana kutokana na mzozo wa kandarasi hivyo akawa mshindi na Julai 4, 2011, alishinda ubingwa wake wa tano mfululizo kwa kula ‘Hot Dogs Buns’ 62.
2012 ilikuwa ushindi wake wa sita mfululizo, alivunja rekodi yake ya 2009 kwa kula ‘Hot Dogs Buns’ 68 na 2013, alitwaa taji lake la saba mfululizo, akila jumla ya ‘Hot Dogs Buns’ 69, na kuvunja rekodi yake ya zamani ya Dunia na 2014, Chestnut alitwaa taji lake la nane mfululizo akila jumla ya ‘Hot Dogs Buns’ 61.
Waswahili wanasema ‘Mpigaji Hupigwa’ ndicho kilichomtokea Chestnut kwani ilipoteza Shindano la “Nathan’s Hot Dog Eating” la mwaka 2015 dhidi ya Matt Stonie lakini Julai 4, 2016, Chestnut ilitetea tena ubingwa wake toka kwa Stonie kwa kula ‘Hot Dogs Buns’ 70 na kuweka rekodi ya juu.
Mwaka mmoja baadaye Julai 4, 2017, aliinyanyua rekodi yake kwa kula ‘Hot Dogs Buns’ 72 na mwaka uliofuata pia akaivunja tena rekodi yake ya Dunia ya kula ‘Hot Dogs Buns’ 74, huku akipata taji la 12 mwaka 2019, kwa ushindi wa kula ‘Hot Dogs Buns’ 71, lakini akishindwa kuivunja rekodi yake ya awali.
Mnamo 2020, alikula ‘Hot Dogs Buns’ 75, na kuweka rekodi ya ulimwengu ya shindano hilo. halafu 2021, akala ‘Hot Dogs Buns’ 76, akivunja rekodi yake ya Ulimwengu kwa shindano hilo, pia mwaka 2022, alipiga ‘Hot Dogs Buns’ 63 ukawa ni ubingwa wake wa 15 na Julai 4, 2023, alitwaa tena taji lake la 16 kwa kula ‘Hot Dogs Buns’ 62.
Wasifu
Joseph Christian Chestnut alizaliwa Novemba 25, 1983, katika Kaunti ya Fulton, Kentucky, na kukulia Vallejo, California akiwa na Shahada ya Uhandisi na Usimamizi wa Ujenzi kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la San Jose, akiwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jimbo la San Jose mwaka 2005, alishiriki shindano la kula Parachichi iliyokaangwa, ambapo alimshinda mlaji wa Daraja la juu, Rich LeFevre kwa kula pauni 6.3 (kilo 2.9) za Parachichi ndani ya dakika 11.5.
Mwaka huo huo, wakati wa Shindano alikula ‘Hot Dogs Buns’ 32, na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Takeru Kobayashi na Sonya Thomas, huku Oktoba 22, 2005, Chestnut ikiweka rekodi mpya ya Dunia ya kuangusha Sandwichi za jibini 32.5 kwa dakika 10 katika Maonyesho ya Jimbo la Arizona na yeye ni Bingwa wa kula wa Kimarekani na hadi kufikia mwaka 2022, ameorodheshwa kuwa ni Bingwa wa kula ulimwenguni.