Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari ya Itega, Mohamed Ramadhani (18) kwa tuhuma za kujihusisha na uhalifu pamoja na kumkaba mama yake mzazi.
Hayo yamesemwa hii leo jijini Dodoma na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Gilles Muroto alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kijana huyo amekuwa akijishughulisha na uhalifu kwa siku za hivi karibuni aliwahi kukiri kumkaba mama yake mzazi lakini mama huyo hakujua kuwa aliyemkaba ni mwanaye.
“Huyu kijana alijua kuwa aliyemkaba na kumpora ni mama yake mzazi, alichofanya ni kumwachia mkoba aliompora na kutokomea kusikojulikana bila yule mama kufahamu, kuwa aliyemkaba ni mwanaye wa kumzaa,” amesema Kamanda Muroto
Aidha, Kamanda Muroto amesema baada ya tukio hilo kijana huyo aliachiwa lakini alikamatwa tena, alipobainika kuwa amehusika katika kuvunja nyumba ya mtu na kuwafunga kamba wenye nyumba ili wawaibie.
-
MNH wazungumzia afya ya Kigwangalla, ujumbe kwa wanahabari
-
Video: Nape, Bashe hawawezi kufukuzwa uanachama- Ridhiwani Kikwete
-
Dkt. Kalemani apiga marufuku TANESCO, REA kuagiza vifaa nje ya nchi
Hata hivyo, kwa upande wake mtuhumiwa huyo amedai chanzo cha yeye kujihusisha na matukio hayo ya uhalifu ni kutokana na hali ngumu ya maisha ndio imemfanya kutenda hayo.
Wengine wanaounda kundi hilo la Kamchape lililopo Kizota ni Abdul Mchangala (18), Mashaka Idd (17), Salum Mohamed (24) na Hamis Kikweli (40).