Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema kuwa imemkamata mtuhumiwa wa biashara ya mihadarati, Ayoub Kiboko jijini hapa.

Kiboko ambaye ni mfanyabiashara maarufu ndani na nje ya nchi anadaiwa kumiliki hoteli kubwa zaidi ya 10 pamoja nyumba za kifahari katika maeneo mbalimbali hapa jijini.

Aidha, Mamlaka hiyo imesema kuwa ilikuwa ikimsaka mtuhumiwa huyo kwa muda mrefu na alikamatwa pamoja na mkewe, Pilli Kiboko Mei 23 saa 8 usiku wakiwa nyumbani kwao eneo la Tegeta.

Kiboko ni miongoni mwa wafanyabiashara waliotajwa katika barua za Watanzania waliofungwa Hong Kong ambazo zililetwa nchini Desemba 2014 na Kasisi, John Wotherspoon anayesaidia wafungwa katika magereza ya Hong Kong na China.

Hata hivyo, Kamishna wa Operesheni DCEA, Frederick Milanzi amesema kuwa walimkamata Kiboko akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin, gramu 250 katika msako uliofanywa nyumbani kwake usiku wa manane.

Samia Suluhu awataka TAWLA kuwasaidia wanawake wajasilia mali

 

Kauli tata za Cristiano Ronaldo zawaweka njia panda mashabiki
Video: Lissu kufanyiwa upasuaji wa mwisho Juni 4, CCM yakanusha katibu wake Kinana kujiuzulu