Kada wa Chadema, Ameri Nkulu amechaguliwa kuwa diwani wa kata ya Lusaka, Sumbawanga wakati akiwa anatumikia kifungo gerezani.

Taarifa za kuaminika kutoka Sumbawanga zimeeleza kuwa Kada huyo wa Chadema alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kupigana hadharani na kiongozi wa CCM katika kata hiyo, Kristian Kafwimbi.

Nkulu alihukumiwa kifungo hicho siku mbili kabla ya zoezi la kupiga kura lakini wananchi wa kata hiyo walimchagua kuwa diwani wao.

Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga, Rozari Mugisa alimhukumu adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria huku alikataa ombi la wakili wa Nkulu kutaka alipe faini ya shilingi 500 kama sheria inavyotoa nafasi hiyo mbadala.

“Kwa mujibu wa sheria, kwa kosa la kupigana hadharani, mtenda kosa anaweza kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya shilingi 500,” Wakili wa kujitegemea Mathias Bododi aliiambia Mwananchi.

Akifafanua kuhusu tukio hilo, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), Emmanuel Kawishe alisema kuwa kwa kuwa Nkulu alihukumiwa kifungo kisichozidi mwaka mmoja anaruhusiwa kuendelea kuwa diwani na kwamba ataapishwa baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake.

 

Kasi ya Magufuli: Kaya Mpya Milioni 1 Kuunganishiwa Maji Safi na Salama Ndani Ya Miezi Sita Ijayo
Cesc Fabregas Awageuka Wachezaji Wenzake