Aliyekua beki wa kushoto wa klabu ya Ashley Cole amewataka mashabiki wa klabu hiyo kumstahamili meneja mpya Unai Emery, baada ya kuanza vibaya ligi kuu ya soka nchini England kwa kupoteza michezo miwiwli ya mwanzo dhidi ya Man City na Chelsea.
Cole ambaye alikua miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi cha Arsenal kilichotwaa ubingwa wa England msimu wa 2003/04 bila kufungwa, amesema meneja huyo kutoka nchini Hispania anahitaji muda wa kufanya mabadiliko baada ya kupokea mikoba kutoka kwa Arsene Wenger aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita.
Coe mwenye umri wa miaka 37, amesema ni vigumu kwa baadhi ya mashabiki kuvumilia hali iliopo kwa sasa, lakini hakuna budi kufanya hivyo, ili kutoa nafasi kwa meneja huyo kuusuka vyema mfumo anaoutumia kikosini na baadae kuanza kupata ushindi.
“Ni vigumu kwa kila shabiki anaeipenda Arsenal kuvumia hali hii, lakini kwa upande wangu ninaamini ni hali ya mpito na muda si mfefu kikosi kitarejea katika hali yake ya ushindani na kufanya vizuri.”
“Tunapaswa kujifunza kutokana na makosa, ninaamini Unai kwa sasa ameshapata funzo na kuitambua ligi ya England, ni ligi ya iana gani, ninatarajia makubwa kutoka kwake, na ninawasilihi mashabiki waendelee kuwa wavumilivu.”
“Suala la kuwa na meneja mpya sio la kutarajia matokeo ya haraka, inabidi uchukue muda wa kujifunza baadhi ya mambo na wachezaji wafahamu vizuri mfumo unaotumiwa na meneja mpya, hivyo itachukua muda mpaka kuona hali ya furaha ya ushindi inarejea miongoni mwa mashabiki.” Alisema Ashley Cole alipohojiwa na gazeti la The Sun.
Katika mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu wa 2018/19 Arsenal walikubali kupoteza kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa kufungwa mabao mawili kwa moja na mabingwa watetezi Man City, kabla ya kupoteza tena mbele ya Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge mwishoni mwa juma lililopita.
Mwishoni mwa juma hili The Gunners wanatarajia kurejea nyumbani Emirates Stadium kucheza mchezo wa mzunguuko wa tatu wa ligi kuu ya England, kwa kuwakabili wagonga nyundo wa jiji hilo West Ham Utd.